Moja ya picha ya pamoja ya Sisi Tanzania pamoja na Jatu plc, waandaaji wa Kongamano la Vijana na Mwalimu Nyerere lililofanyika Jana Tarehe 14/10/2021 Ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete conventional center katika kuadhimisha miaka 22 ya kifo cha Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere, ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkurugenzi wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Mhe. Joseph Butiku, ambaye pia alikuwa Katibu wa Mwl.Nyerere enzi za uhai wake.
Huku akiambatana na Mbunge Kijana wa Dodoma Mjini Mhe. Anthony Mavunde akiambatana na wabunge wengine wakiwemo Mh. Festo Sanga, Mhe. Nusrat Hanje, Mhe. Neema Lugangira, Mhe. Judith Kapinga, Mhe. Humphrey Polepole kuwataja wachache.
Taasisi na mashirika mbalimbali yalihudhuria mkutano huu, wanafunzi wa vyuo, wahadhiri, wanafunzi wa sekondari, wajasiriamali na wananchi wengine.
Copyright © 2025 Developed by sisitanzania.org. All rights reserved.